Msaada Wangu Watoka Wapi?
Wimbo wa kwenda juu.
121 1 Nainua macho yangu niitazame milima—msaada wangu utatoka wapi?
2 Msaada wangu watoka kwa Baba yangu, aliyeziumba mbingu na nchi.
3 Hataiacha mguu wako uteleze; yeye akulindaye hatasinzia. 4 Naam, yeye anayemlinda Israeli hatasinzia wala hatalala.
5 Baba yako anakulinda; Baba yako ni kivuli upande wa mkono wako wa kuume. 6 Jua halitakupiga mchana, wala mwezi wakati wa usiku.
7 Baba yako atakulinda na mabaya yote; atayahifadhi maisha yako. 8 Baba yako atalinda kutoka kwako na kuingia kwako, tangu sasa na hata milele.