Soma. Pokea. Pendekeza.

♥ Maoni

Wimbo Ulio Bora 4

Kitabu

Hakuna Doa Kwako

Mwanamume amsifu mwanamke kiungo baada ya kiungo, amwita bibi-arusi wake na dada yake, asema hakuna dosari ndani yake. Yeye ni bustani iliyofungwa, chemchemi iliyotiwa muhuri, yake peke yake. Mwishoni yeye ajibu, akiuita upepo na kuifungua bustani hiyo mwenyewe.

Sura ya 4.

Tazama, wewe ni mzuri, mpenzi wangu, tazama, wewe ni mzuri! Macho yako ni kama ya njiwa nyuma ya utaji wako. Nywele zako ni kama kundi la mbuzi washukao kwenye miteremko ya Gileadi. Meno yako ni kama kundi la kondoo waliokatwa manyoya karibuni, wakipanda kutoka kuoga, kila mmoja akizaa mapacha, wala hakuna hata mmoja aliyefiwa na mwanawe. Midomo yako ni kama uzi mwekundu, na kinywa chako ni cha kupendeza. Mashavu yako ni kama vipande viwili vya komamanga nyuma ya utaji wako. Shingo yako ni kama mnara wa Daudi, uliojengwa kwa safu za mawe; juu yake hutundikwa ngao 1,000, kila moja ni ngao ya shujaa. Maziwa yako mawili ni kama wana-paa wawili, mapacha wa paa, wakila katika mahali penye maua ya yungiyungi. Hata siku ipumzikapo na vivuli vikimbiapo, nitakwenda mlima wa manemane na kilima cha ubani. Wewe u mzuri kabisa, mpenzi wangu; hakuna doa kwako.

Njoo pamoja nami kutoka Lebanoni, bibi arusi wangu; njoo pamoja nami kutoka Lebanoni. Tazama chini kutoka kilele cha Amana, kutoka kilele cha Seniri na Hermoni, kutoka mapango ya simba, kutoka milima ya makao ya chui. Umeuteka moyo wangu, dada yangu, bibi arusi wangu; umeuteka moyo wangu kwa mtazamo mmoja wa macho yako, kwa kito kimoja cha mkufu wako. Jinsi upendo wako ulivyo mzuri, dada yangu, bibi arusi wangu! Upendo wako ni bora zaidi kuliko divai, na harufu nzuri ya mafuta yako kuliko kiungo chochote! Midomo yako yadondoza asali safi, bibi arusi wangu; asali na maziwa vi chini ya ulimi wako, na harufu nzuri ya mavazi yako ni kama harufu nzuri ya Lebanoni.

Bustani iliyofungwa ndiyo dada yangu, bibi arusi wangu, chemchemi iliyofungwa, kisima kilichotiwa muhuri. Matawi yako ni bustani ya mikomamanga yenye matunda bora kabisa, hina pamoja na nardo, nardo na zafarani, mchai na mdalasini, pamoja na kila mti wa ubani, manemane na udi, pamoja na viungo vyote bora kabisa. a a v14 Mchai ni tete lenye harufu nzuri litumiwalo kama kiungo. Wewe u chemchemi ya bustani, kisima cha maji yaliyo hai, na vijito vitiririkavyo kutoka Lebanoni. Amka, upepo wa kaskazini, na uje, upepo wa kusini! Vuma juu ya bustani yangu, ili viungo vyake vitiririke. Mpenzi wangu na aingie katika bustani yake, na kula matunda yake bora kabisa.

A young man reading the Father's Heart Bible (FHB) print edition in a coffee shop Sasa Imechapishwa

Maoni

Mawazo, maswali, au neno ambalo sura hii imeliamsha ndani yako — lishiriki hapa. Kila maoni huweka jina lako kwenye Wall of Contributors.

Kusoma, kunakili na kushiriki ni wazi kwa kila mtu — huhitaji akaunti. Kutoa maoni, kutia alama, na kuhifadhi mahali ulipofikia hupatikana kwa akaunti ya bure, na kila maoni huweka jina lako kwenye Wall of Contributors.

Jiunge na Familia — ni bure →
  • Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kuchangia.