Kilio cha Daudi cha Kuomba Kuokolewa
Shigayoni ya Daudi, aliyomwimbia Baba yetu kwa habari ya Kushi, Mbenyamini.
Akishtakiwa na Kushi, Mbenyamini, Daudi anaapa kiapo: kama amemlipa rafiki yake ubaya, adui yake na amkanyage hata mavumbini. Anamwomba Baba yake, Mwamuzi achunguzaye mioyo, atende, naye anawaona wenye jeuri wakianguka katika shimo lao wenyewe.
7 1Ee Baba yangu, kwako nakimbilia; niokoe na wote wanaonifuatia, uniponye, 2asije akanirarua kama simba, akinipasua vipande vipande, wala hakuna wa kuokoa. 3Ee Baba yangu, kama nimetenda haya—kama kuna uovu mikononi mwangu, 4kama nimemlipa rafiki yangu kwa uovu, au nimemteka nyara adui yangu bila sababu, 5basi adui na anifuatie na anipate mimi, na aukanyage uhai wangu chini, na kuulaza heshima yangu mavumbini.
6Inuka, Baba yangu, katika hasira yako; simama dhidi ya ghadhabu ya adui zangu; amka kwa ajili yangu—umeamuru hukumu. 7Kusanyiko la mataifa na likuzunguke wewe; keti mahali pa juu juu yao. 8Baba yetu huhukumu mataifa. Nihukumie haki, Baba yangu, sawasawa na haki yangu na sawasawa na ukamilifu ulio ndani yangu. 9Ukomeshe uovu wa waovu, lakini umtegemeze mwenye haki—wewe uchunguzaye nia na mioyo, Ee Baba mwenye haki. 10Ngao yangu ni Baba yangu, awaokoaye wanyofu wa moyo. 11Baba yetu ni mwamuzi mwenye haki, Mungu ambaye ana ghadhabu kila siku. 12Mtu asipotubu, Baba yetu atainoa upanga wake; ameuvuta upinde wake, akauweka tayari. 13Ameandaa silaha zake za mauti; hufanya mishale yake kuwa ya moto uwakao. 14Tazama, mtu mwovu ana mimba ya uovu; hutunga taabu na kuzaa uongo. 15Huchimba shimo na kulifukua, lakini huanguka katika shimo alilolitengeneza. 16Taabu yake humrudia kichwani mwake mwenyewe; jeuri yake humshukia utosini mwake mwenyewe. 17Nitamshukuru Baba yangu kwa ajili ya haki yake, nami nitaliimbia sifa jina la Baba yangu, Aliye Juu.