Kukana kwa Mpumbavu
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
14 1 Mpumbavu amesema moyoni mwake, "Hakuna Mungu." Wameharibika, matendo yao ni maovu; hakuna atendaye mema.
2 Baba yetu huchungulia toka mbinguni juu ya wanadamu, aone kama yuko mtu mwenye akili, amtafutaye. 3 Wote wamepotoka; wameoza wote pia; hakuna atendaye mema, la, hata mmoja.
4 Je, hawajui neno, wote watendao maovu, walao watu wangu kama walavyo mkate, wala hawamwiti Baba yetu? 5 Ndipo waliposhikwa na hofu kuu, kwa maana Baba yetu yu pamoja na kizazi cha wenye haki. 6 Ninyi watenda maovu mngeshinda shauri la maskini, lakini Baba yetu ndiye kimbilio lake.
7 Laiti wokovu wa Israeli ungetoka Sayuni! Baba yetu awarudishiapo watu wake toka utumwani, Yakobo atashangilia, Israeli atafurahi.