Kutoka Vilindini
Wimbo wa kwenda juu.
130 1 Kutoka vilindini nakulilia wewe, Baba yangu.
2 Baba Mwenye Enzi, sikia sauti yangu; tega sikio kwa dua zangu za huruma.
3 Kama wewe, Baba yangu, ungehesabu maovu, Baba Mwenye Enzi, ni nani angeweza kusimama? 4 Lakini kwako kuna msamaha, ili upate kuogopwa.
5 Ninangoja Baba yangu; nafsi yangu inangoja, na katika neno lake naweka tumaini langu. 6 Nafsi yangu inamngojea Baba Mwenye Enzi kuliko walinzi wangojeavyo asubuhi, naam, kuliko walinzi wangojeavyo asubuhi.
7 Ee Israeli, weka tumaini lako kwa Baba yetu, kwa maana kwa Baba yetu kuna upendo wa agano, na kwake kuna ukombozi tele. 8 Naye mwenyewe atamkomboa Israeli na maovu yake yote. a a v8 Ahadi ya Baba ya kuwakomboa watu wake na dhambi zao zote inatimizwa katika Yesu, aliyepewa jina hilo ili kuwaokoa watu wake kutoka dhambi zao.