Wenye mizizi katika Baba
Wimbo wa kwenda juu.
125 1 Wale wanaomtumaini Baba yetu ni kama mlima Sayuni, usioweza kutikiswa bali udumuo milele. 2 Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, ndivyo Baba yetu anavyowazunguka watu wake, tangu sasa na hata milele. 3 Fimbo ya uovu haitakaa juu ya nchi waliyopewa wenye haki, ili wenye haki wasinyooshe mikono yao kutenda mabaya. 4 Uwatendee mema, Baba yetu, wale walio wema, wale walionyoka mioyoni mwao. 5 Bali wale wanaogeukia njia zao zilizopotoka, Baba yetu atawaondoa pamoja na watenda maovu. Amani iwe juu ya Israeli!