Karama Zinazoijenga Familia
Kunena kwa lugha pasipo tafsiri humjenga mnenaji peke yake, basi unabii ni bora: mgeni aingiaye apate kufunuliwa siri za moyo wake na kuanguka chini akiabudu. Kila jambo katika kusanyiko hupimwa kwa kuangalia kama linajenga, nalo hufanyika kwa utaratibu, kwa sababu Baba yetu si wa machafuko.
14 1Fuatieni upendo, na kutamani sana karama za rohoni, lakini hasa mpate kutoa unabii. 2Anenaye kwa lugha hasemi na watu, bali na Baba yetu—kwa maana hakuna mtu amfahamuye—bali kwa Roho anena siri. 3Bali yeye atoaye unabii, huwaambia watu maneno ya kuwajenga, na kuwatia moyo, na kuwafariji. 4Anenaye kwa lugha hujijenga nafsi yake; bali atoaye unabii huijenga kanisa. 5Nataka ninyi nyote mnene kwa lugha, lakini zaidi mtoe unabii. Yeye atoaye unabii ni mkuu kuliko yeye anenaye kwa lugha, isipokuwa afasiri, ili kanisa lipate kujengwa.
6Basi, ndugu zangu, nikija kwenu nikinena kwa lugha, nitawafaa nini, nisipowaambia kwa njia ya ufunuo, au maarifa, au unabii, au mafundisho? 7Hata vitu visivyo na uhai vitoavyo sauti—kama filimbi au kinubi—kama havitoi tofauti ya sauti, jinsi gani mtu atakavyojua kilichopigwa? 8Na tarumbeta ikitoa sauti isiyodhihirika, ni nani atakayejiweka tayari kwa vita? 9Kadhalika na ninyi: msipotamka kwa ulimi maneno yaliyo dhahiri, jinsi gani mtu atakavyojua yaliyonenwa? Kwa maana mtakuwa mkinena hewani tu. 10Zipo lugha za namna nyingi ulimwenguni, bila shaka; wala hakuna hata moja isiyo na maana. 11Basi nisipoijua maana ya sauti, nitakuwa mgeni kwa yeye anenaye, naye anenaye atakuwa mgeni kwangu. 12Kadhalika na ninyi: kwa kuwa mnatamani sana karama za rohoni, tafuteni kuzidi katika kulijenga kanisa. 13Kwa sababu hiyo yeye anenaye kwa lugha na aombe apate kuifasiri. 14Kwa maana nikiomba kwa lugha, roho yangu huomba, lakini akili yangu haina matunda.
15Basi nifanyeje? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia; nitaimba kwa roho, tena nitaimba kwa akili pia. 16Kwa maana ukibariki kwa roho, yeye aketiye mahali pa mgeni atasemaje "Amina" juu ya shukrani yako, kwa kuwa hajui usemalo? 17Wewe wafanya vyema kutoa shukrani, lakini yule mwingine hajengwi. 18Namshukuru Baba yetu kwamba mimi nanena kwa lugha kuliko ninyi nyote. 19Lakini katika kanisa napenda kunena maneno matano kwa akili yangu, nipate kuwafundisha wengine pia, kuliko maneno kumi elfu kwa lugha.
20Ndugu zangu, msiwe watoto katika kufikiri. Kuweni watoto wachanga katika uovu, bali kuweni watu wazima katika kufikiri.
21Katika Torati imeandikwa: "Kwa watu wa lugha ngeni na kwa midomo ya wageni nitasema na watu hawa, wala hata hivyo hawatanisikiliza," asema Baba yetu.
22Basi lugha ni ishara, si kwa waaminio, bali kwa wasioamini; bali unabii ni ishara, si kwa wasioamini, bali kwa waaminio. 23Basi, kanisa lote likikusanyika pamoja, na wote wakinena kwa lugha, na wakiingia watu wasiojua au wasioamini, je! hawatasema kwamba mna wazimu? 24Lakini wote wakitoa unabii, akiingia mtu asiyeamini au asiyejua, hushitakiwa na wote, huhukumiwa na wote, 25siri za moyo wake hufunuliwa; hivyo huanguka kifudifudi na kumsujudia Baba yetu, akikiri kwamba Baba yetu yumo kati yenu kweli kweli.
Ibada kwa Utaratibu Unaostahili
26Basi ni nini, ndugu zangu? Mnapokutana, kila mmoja ana wimbo, ana mafundisho, ana ufunuo, ana lugha, ana tafsiri. Mambo yote na yatendeke kwa kusudi la kujenga. 27Kama mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu kwa uchache, kila mmoja kwa zamu, na mmoja na afasiri. 28Ila kama hakuna mfasiri, na anyamaze kimya katika kanisa, ajinene mwenyewe na kwa Baba yetu. 29Manabii na wanene wawili au watatu, na wengine na wapime kwa uangalifu yaliyonenwa. 30Lakini mtu mwingine aketiye akipata ufunuo, yule wa kwanza na anyamaze. 31Kwa maana ninyi nyote mwaweza kutoa unabii mmoja mmoja, ili wote wapate kujifunza, na wote watiwe moyo, 32nazo roho za manabii huwatii manabii. 33Kwa maana Baba yetu si Mungu wa machafuko, bali wa amani, kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu. 34Wanawake na wakae kimya katika makanisa; kwa maana hawana ruhusa kunena, bali watii, kama vile Torati isemavyo. a a v34 Baadhi ya nakala huweka mistari 34-35 baada ya mstari wa 40. 35Nao wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani; kwa maana ni aibu mwanamke kunena katika kanisa. 36Au je! neno la Baba yetu lilianzia kwenu? Au liliwafikia ninyi peke yenu? 37Mtu akijiona kuwa ni nabii au ni mtu wa rohoni, na aitambue kwamba mambo ninayowaandikia ni amri ya Bwana. 38Lakini mtu akiyapuuza haya, naye mwenyewe atapuuzwa.
39Basi, ndugu zangu, takeni sana kutoa unabii, wala msikataze kunena kwa lugha. 40Lakini mambo yote na yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu.