Kilio cha Uhitaji wa Haraka
Kwa mwimbishaji. Ya Daudi. Kwa kukumbusha.
70 1 Fanya haraka, Baba yangu, kuniokoa! Baba yangu, fanya haraka kunisaidia! 2 Waaibike na kufedheheshwa wale wanaotaka kuniua; wale wafurahiao madhara yangu warudishwe nyuma na kuaibishwa. 3 Wale wasemao, "Aha! Aha!" warudi nyuma kwa sababu ya aibu yao.
4 Lakini wote wakutafutao washangilie na kufurahi ndani yako; wale wapendao wokovu wako waseme daima, "Baba yetu ni mkuu!" 5 Lakini mimi ni maskini na mhitaji; njoo kwangu haraka, Baba yangu! Wewe ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu; Baba yangu, usikawie.