Watawala Waovu
Kwa mwimbishaji: kwa mtindo wa "Usiharibu." Zaburi ya Daudi. Utenzi.
58 1 Je, kweli mnaamua yaliyo haki, enyi watawala? Je, mnawahukumu wanadamu kwa haki? a a v1 "Usiharibu" ni jina la wimbo ambao zaburi hii iliimbwa kwa mtindo wake. 2 La, mioyoni mwenu mnabuni maovu; mikono yenu inaeneza jeuri katika nchi. 3 Waovu wamepotoka tangu tumboni; wamepotea tangu kuzaliwa, wakisema uongo. 4 Sumu yao ni kama sumu ya nyoka, kama fira kiziwi azibaye sikio lake, 5 asije akaisikia sauti ya waaguzi wala ya mchawi mwenye ujanja. 6 Ee Baba yetu, vunja meno vinywani mwao; ng'oa meno makali ya wana simba, Baba yetu! 7 Na watoweke kama maji yapitayo; Baba yetu aelekezapo mishale yake, na wakatike. 8 Kama konokono ayeyukaye aendapo, kama mtoto aliyezaliwa mfu asiyeliona jua. 9 Kabla vyungu vyenu havijahisi joto la miiba, ikiwa mibichi au inayowaka, atawafagilia mbali. 10 Wenye haki watafurahi watakapoona hukumu ikitendeka; wataosha miguu yao katika damu ya waovu. 11 Nao watu watasema, "Hakika kuna thawabu kwa wenye haki; hakika Baba yetu anaihukumu dunia."