Utenzi wa Dhahabu huko Gathi
Kwa mwimbishaji: mtindo wa "Njiwa wa Mialoni ya Mbali." Zaburi ya Daudi. Utenzi wa dhahabu, wakati Wafilisti walipomkamata huko Gathi.
56 1 Unifadhili, Baba yangu, kwa maana watu wananikanyaga; mchana kutwa mshambuliaji ananisonga. 2 Adui zangu wananikanyaga mchana kutwa; wengi wanapigana nami kwa kiburi chao. 3 Ninapoogopa, nitakutumaini wewe.
4 Katika Baba yangu, ambaye neno lake ninalisifu—katika Baba yangu ninatumaini; Sitaogopa. Mwanadamu tu anaweza kunitenda nini? 5 Mchana kutwa wanapotosha maneno yangu; mawazo yao yote dhidi yangu ni mabaya. 6 Wanakusanyika pamoja, wanavizia; wanachunguza hatua zangu, wakitumaini kuutwaa uhai wangu.
7 Je, wataponaje kwa uovu wao? Kwa hasira uwaangushe mataifa, Baba yangu. 8 Umezihesabu kutangatanga kwangu; uyaweke machozi yangu katika chupa yako. Je, hayamo katika kitabu chako?
9 Ndipo adui zangu watarudi nyuma nitakapoita. Hili najua: kwamba Baba yangu yuko upande wangu. 10 Katika Baba yangu ninasifu neno lake; katika Baba yangu ninalisifu neno lake.
11 Katika Baba yangu ninatumaini; sitaogopa. Mwanadamu tu anaweza kunitenda nini? 12 Nadhiri zako ziko juu yangu, Baba yangu; nitakutolea sadaka za shukrani. 13 Kwa maana umeikomboa nafsi yangu na mauti—naam, miguu yangu isijikwae—ili nitembee mbele za Baba yangu katika nuru ya uzima.