Sifa za Daudi kwa Moyo Wote
Zaburi ya Daudi.
138 1 Nitakusifu kwa moyo wangu wote; mbele ya miungu nitakuimbia sifa zako. 2 Nitasujudu kuelekea hekalu lako takatifu nami nitalishukuru jina lako kwa ajili ya upendo wako wa agano na uaminifu wako, kwa maana umelitukuza neno lako kuliko jina lako lote. 3 Siku ile nilipokuita, uliniitikia mimi; ulinitia ujasiri, kwa nguvu nafsini mwangu.
4 Wafalme wote wa dunia watakusifu, Baba yangu, kwa maana wameyasikia maneno ya kinywa chako. 5 Wataziimba njia za Baba yetu, kwa maana utukufu wa Baba yetu ni mkuu. 6 Ijapokuwa Baba yetu ametukuka, huwaangalia wanyenyekevu, bali huwafahamu wenye kiburi kwa mbali.
7 Nijapotembea katikati ya taabu, wewe hunihifadhi hai; unaunyoosha mkono wako dhidi ya ghadhabu ya adui zangu, na mkono wako wa kuume huniokoa. 8 Baba yetu atatimiza kusudi lake kwa ajili yangu; upendo wako wa agano, Baba yangu, wadumu milele. Usiiache kazi ya mikono yako.