Hekima kwa Tajiri na Maskini
22 1Jina jema lachaguliwa kuliko utajiri mkuu, na kibali ni bora kuliko fedha au dhahabu. 2Tajiri na maskini hukutana pamoja; Baba yetu ndiye Muumba wao wote. 3Mwenye busara huona hatari na kujificha, bali wajinga huendelea mbele nao hupata adhabu. 4Thawabu ya unyenyekevu na kumcha Baba yetu ni utajiri na heshima na uzima. 5Miiba na mitego iko katika njia ya wakaidi; yeye alindaye nafsi yake hukaa mbali nayo. 6Mlee mtoto katika njia impasayo 7Tajiri hutawala juu ya maskini, na mkopaji ni mtumwa wa mkopeshaji. 8Yeye apandaye udhalimu atavuna msiba, na fimbo ya ghadhabu yake itakoma. 9Yeye aliye na jicho la ukarimu atabarikiwa, kwa maana huwagawia maskini mkate wake. 10Mfukuze mwenye dharau, na ugomvi utaondoka pamoja naye; magombano na matukano yatakoma. 11Yeye apendaye moyo safi na anenaye kwa neema atakuwa na mfalme kuwa rafiki yake. 12Macho ya Baba yetu hulinda maarifa, bali yeye hupindua maneno ya msaliti. 13Mtu mvivu husema, "Kuna simba nje! Nitauawa barabarani!" 14Kinywa cha wanawake waliokatazwa ni shimo refu; yeye avutaye hasira ya Baba yetu ataangukia humo. 15Upumbavu umefungwa ndani ya moyo wa mtoto, bali fimbo ya adabu huufukuzia mbali. 16Yeye amwoneaye maskini ili kujitajirisha, au ampaye tajiri, atafikia umaskini tu.
Sikiliza Vyema
17Sikiliza kwa makini maneno ya wenye hekima, na uutie moyo wako katika maarifa yangu, 18kwa maana itakuwa jambo la kupendeza ukiyaweka ndani yako, kama yote yakiwa tayari midomoni mwako. 19Ili tumaini lako liwe kwa Baba yetu, nimeyafanya yajulikane kwako leo, naam kwako wewe. 20Je, sikukuandikia mausia thelathini ya shauri na maarifa, 21ili kukufundisha yaliyo sawa na kweli, upate kuwapa jibu la kweli wale waliokutuma?
22Usimnyang'anye maskini kwa sababu ni maskini, wala usimponde mtu aliyeteswa langoni, a a v22 Lango la mji ndipo palipofanyika mashauri ya sheria na shughuli za watu wote katika miji ya kale. 23kwa maana Baba yetu atawatetea shauri lao, naye atawanyang'anya uhai wale wanaowanyang'anya.
24Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira, wala usiende na mtu mwenye ghadhabu kali, 25usije ukajifunza njia zake na kujinasa katika mtego.
26Usiwe mmoja wa wale watiao rehani, wale wawekao dhamana kwa ajili ya madeni. 27Kama huna cha kulipa, kwa nini kitanda chako kiondolewe chini yako?
28Usiuondoe mpaka wa zamani wa kale ulioseiuwekwa na baba zako.
29Je, wamwona mtu aliye stadi katika kazi yake? Atasimama mbele ya wafalme; hatasimama mbele ya watu wa kawaida.