Habari za Uharibifu wa Yerusalemu Zawasili
1 1Maneno ya Nehemia mwana wa Hakalia. Katika mwezi wa Kislevu, mwaka wa ishirini, nilikuwa katika ngome ya Shushani, a a v1 Kislevu ulikuwa mwezi wa tisa wa kalenda ya Kiebrania, ukiangukia mwishoni mwa Novemba hadi Desemba.
2Hanani, mmoja wa ndugu zangu, akaja pamoja na watu kutoka Yuda. Nikawauliza habari za Wayahudi walionusurika, waliobaki kutoka utumwani, na habari za Yerusalemu. 3Wakaniambia, "Mabaki waliobaki kutoka utumwani, huko katika jimbo, wamo katika taabu kuu na aibu. Ukuta wa Yerusalemu umebomoka, na malango yake yameteketezwa kwa moto."
4Niliposikia maneno hayo, niliketi na kulia, nikaomboleza kwa siku nyingi, nikifunga na kuomba mbele za Baba yetu aliye mbinguni. 5Nikasema: Tafadhali, Baba yangu aliye mbinguni, Mungu mkuu na mwenye kutisha, ushikaye agano na upendo thabiti kwa wale wampendao na kushika amri zake, 6sikio lako na lisikilize na macho yako yafumbuke, ili kusikia maombi haya ambayo mimi, mtumishi wako, ninaomba mbele zako sasa, mchana na usiku, kwa ajili ya Israeli, watumishi wako—nikiziungama dhambi ambazo sisi Waisraeli tumekutenda. Mimi na nyumba ya baba yangu tumefanya dhambi. 7Tumekukosea sana, kwa kutozishika amri, na sheria, na hukumu ulizomwamuru mtumishi wako Musa.
8Tafadhali kumbuka agizo lako kwa mtumishi wako Musa: "Kama mtakuwa si waaminifu, nitawatawanya kati ya mataifa, 9lakini kama mkinirudia mimi, na kushika amri zangu, na kuzitenda, hata kama watu wenu waliohamishwa wako mpaka mwisho wa mbingu, nitawakusanya kutoka huko na kuwaleta mahali nilipopachagua ili jina langu likae huko."
10Hao ni watumishi wako, na watu wako, uliowakomboa kwa uweza wako mkuu na kwa mkono wako wenye nguvu. 11Tafadhali, Baba yangu Bwana Mwenyezi, sikio lako na lisikilize maombi ya mtumishi wako, na maombi ya watumishi wako—wale wapendezwao kuliogopa jina lako. Umfanikishe mtumishi wako leo, na umjalie kupata rehema mbele ya mtu huyu. Wakati huo nilikuwa mnyweshaji wa mfalme.