Mjumbe wa Baba yetu huko Bokimu
2 1Mjumbe wa Baba yetu akapanda kutoka Gilgali mpaka Bokimu, akasema, "Niliwapandisha kutoka Misri hata nchi niliyowaapia baba zenu. Nikasema, 'Sitavunja kamwe agano langu nanyi. 2Nanyi hamtafanya agano na watu wa nchi hii; bomoeni madhabahu zao.' Lakini hamkuisikiliza sauti yangu. Mmefanya nini? 3Basi sasa nasema: Sitawafukuza mbele yenu; watakuwa miiba mbavuni mwenu, na miungu yao itakuwa mtego kwenu."
4Ikawa mjumbe wa Baba yetu alipowaambia maneno haya Waisraeli wote, watu waliinua sauti zao wakalia. 5Wakapaita mahali pale Bokimu, na huko wakamtolea Baba yetu dhabihu. a a v5 Bokimu maana yake ni "waliao" — watu waliyapa mahali hapo jina hilo kwa sababu ya kilio kilichotokea walipoposikia jinsi walivyokuwa wamejitenga mbali na Baba yao.
Kizazi cha Yoshua Chapita
6Yoshua alipowaaga watu, Waisraeli kila mmoja alikwenda kuurithi urithi wake wa nchi. 7Watu wakamtumikia Baba yetu siku zote za Yoshua, na siku zote za wazee walioishi baada yake, ambao walikuwa wameyaona matendo yote makuu ambayo Baba yetu aliwatendea Israeli. 8Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Baba yetu, akafa akiwa na umri wa miaka mia na kumi. 9Wakamzika katika nchi ya urithi wake huko Timnath-heresi, katika nchi ya vilima ya Efraimu, upande wa kaskazini wa mlima Gaashi.
Kizazi Chamsahau Baba
10Nacho kizazi kile chote kikakusanywa pamoja na baba zao, na kikainuka kizazi kingine baada yao ambacho hakikumjua Baba yetu wala kazi aliyoifanya kwa ajili ya Israeli. 11Watu wa Israeli wakafanya maovu machoni pa Baba yetu, wakaitumikia Mabaali. 12Wakamwacha Baba yetu, Mungu wa baba zao, aliyewatoa katika nchi ya Misri. Wakaifuata miungu mingine ya watu waliowazunguka, wakaisujudia, na kumkasirisha Baba yetu. 13Wakamwacha Baba yetu, wakamtumikia Baali na Maashtorethi. 14Basi hasira ya Baba yetu ikawaka juu ya Israeli, akawatia mkononi mwa watekaji nyara waliowateka nyara, akawauza kwa adui waliowazunguka, hata wasiweze tena kusimama mbele yao. 15Kila walipotoka kwenda vitani, mkono wa Baba yetu ulikuwa juu yao kwa mabaya, kama alivyokuwa amewaambia na kuwaapia. Wakawa katika dhiki kuu.
16Ndipo Baba yetu akawainua waamuzi waliowaokoa kutoka mkononi mwa watekaji nyara wao. 17Lakini hawakuwasikiliza hata waamuzi wao. Wakajitia uzinzi kwa kuifuata miungu mingine na kuisujudia, wakageuka upesi kuiacha njia waliyoiendea baba zao, waliozitii amri za Baba yetu; wao hawakufanya vivyo hivyo. 18Baba yetu alipowainua waamuzi, alikuwa pamoja na kila mwamuzi, akawaokoa kutoka mkononi mwa adui zao siku zote za yule mwamuzi; kwa maana Baba yetu alisukumwa na huruma kwa sababu ya kuugua kwao chini ya wale waliowaonea. 19Lakini yule mwamuzi alipokufa, wakageuka nyuma, wakaharibika zaidi kuliko baba zao, wakiifuata miungu mingine ili kuitumikia na kuisujudia. Hawakuacha lo lote katika matendo yao wala njia zao za ukaidi.
20Basi hasira ya Baba yetu ikawaka juu ya Israeli, akasema, "Kwa sababu taifa hili limelivunja agano langu nililowaamuru baba zao, na hawakuisikiliza sauti yangu, 21mimi nami sitalifukuza tena taifa lo lote katika mataifa aliyoyaacha Yoshua alipokufa, 22ili kwa hayo niwajaribu Israeli: kama watazishika njia za Baba yetu, wakizitembea kama baba zao walivyofanya, au sivyo."
23Basi Baba yetu akayaacha mataifa hayo, bila kuyafukuza upesi, wala hakuyatia mkononi mwa Yoshua.