Soma. Pokea. Pendekeza.

♥ Maoni

Ayubu 23

Kitabu

Laiti Ningeweza Kumpata

Sura ya 23.

Ndipo Ayubu akajibu: "Hata leo malalamiko yangu ni machungu; mkono wake ni mzito juu ya kuugua kwangu. Laiti ningejua pa kumpata, ili nifike hata makao yake! Ningeweka mashtaka yangu mbele zake na kujaza kinywa changu hoja. Ningejifunza maneno ambayo angenijibu na kuelewa yale ambayo angeniambia. Je, angeshindana nami kwa ukuu wa nguvu zake? La—bila shaka angenisikiliza. Hapo mtu mnyofu angeweza kuhojiana naye, nami ningeachiliwa huru milele na mwamuzi wangu. Lakini niendapo mashariki, hayupo; nami magharibi siwezi kumpata. Afanyapo kazi kaskazini, siwezi kumwona; ageukapo kusini, siwezi kumpata. Lakini yeye anaijua njia niiendeayo; atakaponijaribu, nitatoka kama dhahabu. Mguu wangu umeshika nyayo zake; nimeishika njia yake wala sikugeuka kando. Sikuiacha amri ya midomo yake; nimeyathamini maneno ya kinywa chake kuliko chakula changu cha kila siku. Lakini yeye habadiliki—ni nani awezaye kumzuia? Chochote akitakacho, hukifanya. Kwa maana atatimiza yale aliyoniagizia, na mambo mengi kama hayo yamo moyoni mwake. Ndiyo sababu ninatetemeka mbele zake; niyafikiripo, ninamwogopa. Mungu ameufanya moyo wangu kuzimia; Mwenyezi amenitia hofu. Lakini sikunyamazishwa na giza, wala na kiza kinene kinifunikacho uso wangu."

A young man reading the Father's Heart Bible (FHB) print edition in a coffee shop Sasa Imechapishwa

Maoni

Mawazo, maswali, au neno ambalo sura hii imeliamsha ndani yako — lishiriki hapa. Kila maoni huweka jina lako kwenye Wall of Contributors.

Kusoma, kunakili na kushiriki ni wazi kwa kila mtu — huhitaji akaunti. Kutoa maoni, kutia alama, na kuhifadhi mahali ulipofikia hupatikana kwa akaunti ya bure, na kila maoni huweka jina lako kwenye Wall of Contributors.

Jiunge na Familia — ni bure →
  • Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kuchangia.