Ayubu Anawajibu Rafiki Zake
13 1"Tazama, jicho langu limeona haya yote; sikio langu limesikia na kuyafahamu. 2Mnayoyajua ninyi, mimi nayajua pia; mimi si duni kwenu. 3Lakini ningesema na Mwenyezi, nami natamani kuiteta hoja yangu na Mungu. 4Bali ninyi mnapaka uongo; nyote ni matabibu wasiofaa kitu. 5Laiti mngenyamaza kimya kabisa— hiyo 6Sasa sikilizeni hoja yangu, na kuisikia dua ya midomo yangu. 7Je, mtasema kwa uongo kwa ajili ya Mungu na kunena kwa udanganyifu kwa ajili yake? 8Je, mtampendelea? Je, mtaiteta hoja kwa ajili ya Mungu? 9Je, ingekuwa vyema kwenu atakapowachunguza? Au mngeweza kumdanganya kama mnavyoweza kumdanganya mwanadamu? 10Hakika atawakemea ikiwa kwa siri mnaonyesha upendeleo. 11Je, adhama yake haitawatia hofu, na utisho wake usiwaangukie? 12Mithali zenu ni methali za majivu; ngome zenu ni za udongo.
13"Nyamazeni mbele yangu, nami niseme; kisha na yaje juu yangu yatakayonijia. 14Kwa nini niuhatarishe mwili wangu mwenyewe na kuutwaa uhai wangu mikononi mwangu mwenyewe? 15Ijapokuwa ataniua, nitamtumaini; lakini nitazitetea njia zangu mbele za uso wake. a a v15 Hata katika kilio chake, tumaini la Ayubu linaelekea kwa Mungu. Mafanikio kamili ya uhusiano yanakuja baadaye — Ayubu anamwona Baba yetu uso kwa uso mwishoni mwa kitabu. 16Hili pia litakuwa wokovu wangu, kwa maana hakuna mtu asiyemcha Mungu angethubutu kuja mbele zake. 17Sikilizeni kwa makini maneno yangu; tangazo langu na lifikie masikio yenu. 18Tazama, nimeitayarisha hoja yangu; najua ya kuwa nitahesabiwa haki. 19Ni nani atakayeteta nami? Kwa maana ndipo ningenyamaza na kufa.
20"Nijalie mambo mawili tu, ndipo sitajificha na uso wako: 21Uondoe mkono wako mbali nami, wala usiache utisho wako unitie hofu. 22Kisha ita, nami nitajibu; au niache niseme, nawe unijibu. 23Makosa yangu na dhambi zangu ni ngapi? Nionyeshe uasi wangu na dhambi yangu. 24Kwa nini unauficha uso wako na kunihesabu kuwa adui yako? 25Je, utalitisha jani lipeperushwalo na upepo na kulifukuza kapi kavu? 26Kwa maana unaandika mambo machungu dhidi yangu na kunirithisha dhambi za ujana wangu. 27Waitia miguu yangu katika mkatale na kuziangalia njia zangu zote; waweka mpaka kwa nyayo za miguu yangu.
28"Basi mwanadamu hudhoofika kama mti unaooza, kama vazi lililoliwa na nondo."