Baba yetu Anena
20 1Ndipo Baba yetu akanena maneno haya yote:
2"Mimi ni Baba yenu, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.
3"Usiwe na miungu mingine mbele yangu.
4"Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho mbinguni juu, wala kilicho duniani chini, wala kilicho majini chini ya nchi. 5Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Baba yenu, ni Baba mwenye wivu, nikiwapatiliza wana dhambi ya wazazi hata kizazi cha tatu na cha nne cha wale wanaonichukia, 6lakini nikiwaonyesha upendo wa agano maelfu ya wale wanaonipenda na kuzishika amri zangu.
7"Usilitaje bure jina la Baba yenu, kwa kuwa Baba yetu hatamhesabu kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.
8"Ikumbuke siku ya Sabato, uitakase. 9Siku sita utafanya kazi na kutenda shughuli zako zote, 10lakini siku ya saba ni Sabato ya Baba yenu. Siku hiyo usifanye kazi yoyote—wewe, wala mwanao wa kiume, wala binti yako, wala mtumishi wako wa kiume au wa kike, wala mnyama wako, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. 11Kwa maana kwa siku sita Baba yetu aliziumba mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, kisha akapumzika siku ya saba; kwa hiyo Baba yetu akaibariki siku ya Sabato akaitakasa.
12"Waheshimu baba yako na mama yako, ili siku zako ziwe nyingi katika nchi akupayo Baba yetu.
13"Usiue.
14"Usizini.
15"Usiibe.
16"Usimshuhudie jirani yako ushahidi wa uongo.
17"Usiitamani nyumba ya jirani yako. Usimtamani mke wa jirani yako, wala mtumishi wake wa kiume au wa kike, wala ng'ombe wake au punda wake, wala kitu chochote alicho nacho jirani yako."
18Watu wote wakaziona ngurumo, na miali ya umeme, na sauti ya baragumu, na mlima ukitoa moshi. Walipoyaona, wakatetemeka, wakasimama mbali.
19Wakamwambia Musa, "Sema wewe nasi, nasi tutasikia. Lakini Baba yetu asiseme nasi, tusije tukafa."
20Musa akawaambia watu, "Msiogope; kwa maana Baba yetu amekuja ili kuwajaribu, na hofu yake iwe pamoja nanyi, msije mkatenda dhambi." 21Watu wakasimama mbali, naye Musa akalikaribia lile giza zito alimokuwako Baba yetu.
Musa Anasogea Karibu
22Ndipo Baba yetu akamwambia Musa, "Waambie wana wa Israeli: Ninyi wenyewe mmeona ya kuwa nimesema nanyi kutoka mbinguni. 23Msifanye miungu ya fedha kando yangu, wala msijifanyie miungu ya dhahabu. 24Nifanyie madhabahu ya udongo, na juu yake utoe dhabihu zako za kuteketezwa na sadaka zako za amani, kondoo zako na ng'ombe zako. Kila mahali nitakapolifanya jina langu likumbukwe, nitakujia na kukubariki. 25Nawe ukinifanyia madhabahu ya mawe, usijenge kwa mawe yaliyochongwa, kwa kuwa ukitumia chombo chako juu yake, unayanajisi. 26Wala usipande madhabahuni kwangu kwa ngazi, uchi wako usije ukafunuliwa juu yake."