Baba yetu Aimarisha Nyumba ya Daudi
14 1Hiramu mfalme wa Tiro akatuma wajumbe kwa Daudi, pamoja na magogo ya mierezi, waashi, na maseremala, ili wamjengee nyumba. 2Daudi akajua ya kuwa Baba yetu alikuwa amemfanya mfalme juu ya Israeli, kwa maana ufalme wake uliinuliwa juu kwa ajili ya watu wake Israeli.
3Naye Daudi akaoa wake wengi zaidi huko Yerusalemu, akazaa wana na binti wengi zaidi. 4Haya ndiyo majina ya watoto aliozaliwa huko Yerusalemu: Shamua, Shobabu, Nathani, na Sulemani, 5Ibhari, Elishua, Elpeleti, 6Noga, Nefegi, Yafia, 7Elishama, Beeliada, na Elifeleti.
Baba yetu Awapasua Wafilisti
8Wafilisti waliposikia ya kuwa Daudi ametiwa mafuta kuwa mfalme juu ya Israeli wote, wote wakapanda kumtafuta Daudi. Daudi akasikia, akatoka kwenda kukabiliana nao. 9Basi Wafilisti walikuwa wamekuja na kuvamia Bonde la Warefai.
10Daudi akamwuliza Baba yetu, "Je, nipande kupigana na Wafilisti? Je, utawatia mkononi mwangu?" Basi Baba yetu akamwambia, "Panda, nami nitawatia mkononi mwako."
11Wakapanda mpaka Baal-perasimu; Daudi akawapiga huko. Daudi akasema, "Baba yetu amewapasua adui zangu kwa mkono wangu kama mafuriko yapasuayo." Kwa hiyo wakapaita mahali pale Baal-perasimu. a a v11 Baal-perasimu maana yake "Bwana apasuaye." 12Nao Wafilisti wakaiacha miungu yao huko, naye Daudi akatoa amri, ikateketezwa kwa moto.
13Wafilisti wakavamia bonde lile tena mara nyingine.
14Daudi akamwuliza Baba yetu tena, naye Baba yetu akasema, "Usipande kuwafuata. Wazingire, umwendee kutoka mkabala wa miti ya miforsadi. 15Utakaposikia sauti ya maandamano katika ncha za miti ya miforsadi, ndipo utakapotoka kwenda vitani—kwa maana Baba yako ametangulia mbele yako kuwapiga jeshi la Wafilisti."
16Daudi akafanya kama Baba yetu alivyomwamuru, nao wakalipiga jeshi la Wafilisti tangu Gibeoni mpaka Gezeri. 17Sifa za Daudi zikaenea katika nchi zote, naye Baba yetu akayafanya mataifa yote yamwogope.